1. Marejesho ya fedha
Mteja akiamua kusitisha mpango wa Lipa Kidogo, atarudishiwa fedha alizolipa ila asilimia 30% itakatwa kama gharama za usumbufu na utawala. Asilimia hii inaweza kuongezeka kutokana na makato ya mtandao husika (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa). Mteja msumbufu anaweza asirudishiwe fedha kabisa.
2. Mabadiliko ya bidhaa & Muda
Kubadilisha bidhaa baada ya kuanza malipo kunaruhusiwa tu kama umetoa taarifa angalau wiki moja (siku 7) kabla ya kupokea bidhaa.
Malipo yanatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliokubaliwa. Hata hivyo, lengo letu ni kumsaidia mteja kupata bidhaa:
- Mteja anaweza kuomba kuongezewa muda endapo atatoa taarifa mapema.
- Maombi yatapitiwa na kukubaliwa kulingana na mawasiliano na makubaliano.
3. Uhifadhi wa Bidhaa
Mteja akipewa taarifa na akakaa kimya kwa muda wa wiki 3 hadi nne, mzigo ukipotea, jukumu linakuwa la mteja.
4. Uwajibikaji wa Mteja
- Mteja anawajibika kufuatilia mpango wake wa malipo.
- Ni muhimu kutoa taarifa mapema kwa mabadiliko yoyote.
5. Haki ya Biashara
- Biashara ina haki ya kusimamia upatikanaji wa bidhaa kulingana na stock iliyopo.
- Masharti haya yanaweza kubadilishwa bila taarifa ya awali.
MUHIMU
Kwa kuanza kulipa, unathibitisha kuwa umesoma, umeelewa na umekubaliana na masharti haya.